Kiungo wa Klabu ya Simba na Timu ya Taifa ya Zambia, Clatous Chama (29) amefiwa na mke wake, Mercy Chama, nchini Zambia.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Wakala wa mchezaji huyo imeeleza kuwa;

“Ni majonzi makubwa, tunasikitika kutangaza kifo cha mke wa mchezaji Clatous Chama, Mercy Mukuka Chama.

“Mercy hakuwa tu mke wa mteja wetu lakini alikuwa sehemu ya familia yetu.

“Tunapenda kutoa salam za pole kwa familia ya Chama na Mukuka, Mungu awape nguvu na faraja,” imesema taarifa hiyo.

CDF Mabeyo atembelea Ubalozi wa Tanzania -Pretoria, asisitiza usimamizi dira ya diplomasia
Mtoto wa siku 7 aibiwa hospitalini