Kiungo Mshambuliaji kutoka Zambia Clatous Chama ameanza mazoezi na wachezaji wenzake wa Simba Sc.

Chama amerejea nchini baada ya kumaliza shughuli za msiba wa mke wake, na huenda akacheza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City kesho Jumanne, Juni 22, jijini Dar es salaam.

Kiungo huyo fundi mwenye uwezo mkubwa wa kufanya vitu bora anapokuwa na mpira aliwasili nchini Jumapili usiku na leo Jumatatu aliamkia katika mazoezi ya timu hiyo.

Chama alianza kufanya mazoezi mepesi na wenzake lakini baadae kocha wa viungo, Adel Zrane alimchukua na kwenda nae pembeni kufanya mazoezi yao binafsi.

Simba SC inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha alama 70, kesho Jumanne itacheza dhidi ya Mbeya City, kisha itakwenda mjini Songea mkoani Ruvuma kucheza mchezo wa Kombe la Shirikishi ASFC dhidi ya Azam FC, mwiahoni mwa juma hili.

Baada ya mchezo huo itarejea jijini Dar es salaam kjkipiga dhidi ya mtani wake Young Africans Julai 03.

RC Makalla atoa siku 2 wezi wa mafuta kujisalimisha
Mbise afunguka ya moyoni