Kiungo kutoka nchini Zambia Clatous Chotta Chama, amesema yupo tayari kurejea kwa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, endapo atatakiwa kufanya hivyo.

Chama aliyecheza Simba SC kwa misimu mitatu kuanzia 2018 hadi 2021, msimu huu amejiunga na RS Berkane ya Morocco.

Akiwa Simba SC, kiungo huyo alipata mafanikio makubwa ikiwemo kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2019/20 na kiungo bora 2020/21.

Simba msimu huu imeanza kwa kasi ya kawaida huku kati ya upungufu ambao umekuwa ukibainishwa ni kukosekana kwa Chama na Luis Miquissone ambao waliondoka mwishoni mwa msimu uliopita.

Akizungumzia uwezekano wa kurudi Simba, Chama alisema: “Simba ikinihitaji nitarudi kuja kufanya nao kazi maana Simba ni klabu nzuri sana na ninaipenda.”

“Inaniuma sana kuona Simba inapata matokeo mabaya kwa sasa maana mimi siku zote nawaombea kheri na mafanikio kama wao wanavyo niombea,” amesema Chama na kuongeza

“Kama ningekutana na Simba kwenye michuano ya kimataifa na nikafunga basi ingetegemea, nisingetamani kushangilia.”

Konde Gang wamrudisha Ibraah Mtwara
Kocha Nabi aisoma Namungo FC kwa Mkapa