Kioungo kutoka nchini Zambia Clatous Chama ameshindwa kuondoka jijini Dar es salaam leo Jumatatu (Julai 17) kuelekea nchini Uturuki kujiunga na wachezaji wenzake kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu ujao 2023/24.

Chama alitakiwa kuondoka sambamba na wachezaji wenzake Jean Baleke, Willy Onana na Che Malone lakini imeshindikana kufuatia ishu yake, kwani kesho ana kikao kingine na mabosi wa Simba SC.

Chama aliyezua taharuki baada ya kuelezwa ametikisa kiberiti akitaka kuboreshewa masilahi kama makubaliano waliyoingia na uongozi aliporejea kutoka RS Berkane ya Morocco akipewa mkataba wa miaka miwili na nusu kabla ya kupunguzwa kwa kilichoelezwa ilitokana na kiwango na majeraha aliyokuwa nayo, alikutana viongozi Ijumaa (Julai 14), lakini muafaka haujapatikana.

“Chama atakutana na viongozi Jumanne (Julai 18) kuendelea kujadili ishu yake, hivyo ni ngumu kuondoka na wenzake, huenda atasafiri Alhamisi akiwa na wachezaji wengine akiwamo Luis kwenda kuongeza nguvu kambini,” kimesema chanzo hicho na kuongeza;

“Jean Baleke, Willy Onana na Che Malone hawa ndio nina uhakika wameondoka leo Jumatatu, lakini kwa Chama nadhani ni baada ya kikao na viongozi wa Simba SC kinachofanyika kesho Jumanne.”

Viongozi wa Simba SC wamekuwa wakitafutwa kwa njia ya simu, lakini simu zao zinata bila kupokelewa na hata wakitumiwa ujumbe ili kutoa ifafanuzi wa baadhi ya mambo hayo hawakuwa tayari kujibu. Simba SC, Azam FC, Young Africans na timu nyingine ziko katika maandalizi ya msimu ujao.

TFF yazikumbusha Simba, Azam, Young Africans
Uli Hoeness: Harry Kane atacheza Bayern Munich