Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Elisha Osati, amesema wanafanya uchambuzi ili kubaini tiba mbadala ikiwepo ‘nyungu’ ambazo zimetumika kwenye mapambano ya virusi vya ugonjwa wa Corona.
Dk. Osati ameyasema hayo wakati akitoa tathimini ya kitaalamu kuhusiana na hali ya ugonjwa wa Corona.
Amesema tathimini waliyoifanya kuhususiana na Corona wabebaini idadi ya wagonjwa imepungua kwa kiasi kikubwa katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma wakiwemo wanaohitaji kuwekewa huduma ya Oksijeni.
“Watu walikuwa wanatumia tangawizi, limao ambavyo vina vitamini C na pia inasaidia kwa wingi kujenga kinga za mwili ili kupambana na wadudu mbalimbali wakiwamo virusi vya Corona,”
Dk Osati amesema hawawezi kudharau njia mbadala kwa sababu Watanzania wengi wanapenda kutumia vitu vya miti shamba.
Mtuhumiwa mkuu mauaji ya Kimbari akana mashtaka “sijaua Watusi wowote”
Hata hivyo amesema kitendo cha Watanzania kunawa mikono kila wakati pamoja na kuvaa barakoa kwa mfululizo wa wiki tatu wanaamini njia hio imesaidia kupunguza maambukizi ya Corona.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa kwa kuwa bado haujamalizika.
Serikali yatoa sababu kuchelewa uzalishaji sukari kiwanda cha Mkulazi