Kiungo Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Clatous Chotta Chama ameingia katika sakata la fununu za usajili wa Luis Jose Miquissone anayetajwa kuwa mbioni kuondoka Al Ahly mwishoni mwa msimu huu.
Miquissone anatajwa kuwa kwenye mpango huo, kufuatia kushindwa kuingia kwenye mfumo wa kocha Pitso Mossimane, tofauti na alivyotarajiwa aliposajiliwa akitokea Simba SC mwanzoni mwa msimu huu.
Chama ameingia katika sakata hilo alipokua akijibu masali ya mashabiki wake kupitia mtandao wa Instagram ‘IG Q&A’ akiwa nchini kwao Zambia, kwenye kambi ya timu ya taifa ya taifa hilo ‘Chipolopolo’.
Kiungo huyo aliulizwa na baadhi ya mashabiki wake kupitia mtandao huo “Anafuatilia tetesi za rafiki yake Miquissone, na anamiss nini kutoka kwa mchezaji huyo anayecheza nafasi ya Kiungo Mshambuliaji?”
Chama alijibu atafurahi sana endapo atacheza tena na Mchezaji huyo kutoka nchini Msumbuji, baada ya kutengana naye mwanzoni mwa msimu huu wakitokea Simba SC.
“Nitafurahi sana kucheza tena na Miquissone, akirudi Simba SC.” alijibu chama kupitia IG Q&A.
Chama alirejea Simba SC wakati wa Dirisha Dogo la Usajili mwezi Januari 2022, baada ya kuvunja mkataba na klabu ya RS Berkane ya Morocco iliyomsajili mwanzoni mwa msimu huu chini Kocha Florent Ibenge.