Wakati Uganda ikiwa inajiandaa na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka 2016, Mkali wa ‘Tubonge’ Jose Chameleone ameweka msimamo wake hadharani na kutoa sababu zinazompelekea kumuunga mkono rais Yowel Museven wakati kukiwa na changamoto nyingi kwenye.

Akiongea na NTV Uganda wiki iliyopita, Chameleone aliwaambia mashabiki wake kuwa huo ni uamuzi binafsi licha kuwa kuna matatizo mengi kwenye kiwanda cha muziki nchini humo ambapo suala la hati miliki linatajwa kuwa tatizo kubwa la wasanii ambalo serikali ya Museven haijalifanyia kazi.

“Matatizo niliyonayo ni zaidi ya milioni 400 za Rais Museven alizowapa wasanii, naweka rehani hapa… mimi pia ninayo haki, namjua Besigye, namjua Amama lakini mtu wangu ni Museven,” alisema Chameleone.

Chameleone aliutetea uamuzi wake ambao unaonekana kuwa unapingwa na baadhi ya wasanii wakubwa ambao hawamuungi mkono rais huyo. Alisema uamuzi wake ni msimamo binafsi kama alivyosimama wakati baba yake alipomkataza asimuone Daniella Atim lakini alifanya hivyo.

“Baba alinitaka nioe mwanamke kutoka Buganda, niliweka msimamo wangu na nikamwambia baba huyu ndiye wangu na hilo lilikuwa chaguo langu,” alisema.

Matokeo Jimbo la Kawe, Ubungo, Kigamboni na kuhusu Kibamba kwa Mnyika
CUF Wajibu Baada Ya CCM Kudai Wamehujumiwa Uchaguzi Zanzibar