Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi  Dkt. Leonard Chamuriho amewataka watumishi wa wizara Ujenzi na Uchukuzi kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi ili kuongeza ufanisi.

Akizungumza na menejimenti ya Sekta ya Ujenzi na Uchukuzi mara baada ya kuwasili  ofisini hapo jijini Dodoma, Chamuriho ameitaka menejimenti kuunganisha wafanyakazi wa sekta zote kufanya kazi kwa kuzingatia matokeo yanayopimika.

“Jipangeni kuhakikisha kuwa watumishi wote wanafanya kazi kwa umoja na ushirikiano ili kufikia malengo yanayotarajiwa na Serikali katika kuboresha miundombinu nchini,” amesema Mhandisi Chamuriho.

Chamuriho amemtaka Katibu Mkuu-Ujenzi Arch. Elius Mwakalinga na Kaimu Katibu  Mkuu Uchukuzi Gabriel Migire kuhakikisha miradi yote inayoendelea ujenzi wake unakamilika kwa wakati na tija.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ameitaka menejimenti ya Wizara kuweka ratiba ya mara kwa mara ya kukagua miradi ili kupata taarifa ya maendeleo na kuchukua hatua mapema kwa miradi yenye changamoto.

Akiwakaribisha Waziri na Naibu Waziri, Katibu Mkuu Ujenzi amewahakikishia viongozi hao ushirikiano kati yao menejimenti na watumishi kwa sekta anazosimamia.

Tanzania,Hungary zasaini ufadhili wanafunzi wa Kitanzania
Mambo ya nje wamhakikishia ushirikiano Olenasha