Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo itatupa karata yake ya kwanza kwenye Fainali za Mataifa Bingwa Barani Afrika ‘CHAN’ zinazoendelea nchini Cameroon.

Taifa Stars iliyopangwa kundi D, itacheza dhidi ya Zambia kwenye uwanja wa Limbe, nchini Camaroon mishale ya saa moja jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Kuelekea pambano hilo, kocha mkuu wa Taifa Stars Ettiene Ndayiragije, amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huo, ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini Tanzania.

“Kila kitu kipo sawa na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu wa leo ambao utakuwa na ushindani mkubwa ndani ya uwanja,”

“Kazi yetu ni kuona kwamba tunaanza vizuri kwenye mchezo wetu ili kufikia malengo ya kufanya vizuri mechi zetu ambazo tutacheza.” Amesema Ndayiragije.

Stars imepangwa kundi D ikiwa na timu ya Guinea, Zambia na Namibia ambapo leo chezo wake wa kwanza itakuwa dhidi ya Zambia.

Nahodha wa timu ya Taifa ya Zambia, Adrian ‘Acha’ Chama akiwa na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, John Raphael Bocco wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao cha kabla ya mchezo wa leo Zambia Vs Tanzania.
Pawasa auanika hadharani udhaifu wa Kisinda
Kiekie kuongeza nguvu Simba SC

Comments

comments