Haruna Juma, Mpanda – Katavi.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amefungua Tamasha la wiki ya Mwanakatavi huku akitoa wito kwa Wananchi kutumia nafasi hiyo, kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo Mkoa wa Katavi.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa Tamasha hilo, RC Mrindoko amesema Wiki ya Mwanakakatavi inatoa nafasi kwa Wananchi kutumia fursa zilizopo Mkoani humo kwenye Sekta ya Utalii, Kilimo, Madini, Mifugo n.k.

Amesema, shabaha ya Tamasha hilo ni kuhakikisha fursa mbalimbali zinajulikana kwa Wananchi wa ndani na nje ya Katavi, kwa kutoa fursa ya wahudhuriaji kupata elimu mbalimbali kuhusu uwekezaji kutoka kwa watalamu wa Sekta husika.

Tamasha la Wiki ya Mwanakatavi linaloandaliwa katika Viwanja vya Chama cha Mapinduzi – CCM, Azimio mjini Mpanda, linafanyika kwa wiki nzima na tayari limeanza hapo jana Oktoba 25, 2023 na linatarajia kufungwa Oktoba 31, 2023.

Vyeti 190 miradi tathmini ya Mazingira vyatolewa
Idadi ya waliofariki ajali ya Vigwaza yaongezeka