Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi  imelazimika kutoa  mafunzo kwa wadhibiti ubora wa shule 1,469 ili kuondoa tatizo la wanafunzi wanaomaliza shule wakiwa hawajui kusoma na kuandika.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa idara ya uthibiti ubora wa shule bi .Merisera Wasena alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam, amesema baada ya kufanya utafiti katika shule za msingi 6,831 wamebaini idadi hiyo ya wanafunzi wasiojua kusoma wala kuandika katika shule 515 huku wasichana wakiwa ni 5, 263 na wavulana ni 5010.

Merisela aliongeza kuwa, hatua  iliyochukuliwa kwa sasa ni kupitia mpango wa ufundishaji na ujifunzaji wa kusoma, kuandika na kuhesabu KKK chini ya mtaala wa shule za msingi kwa darasa la kwanza na darasa la pili litawawezesha wanafunzi kufika darasa la nne wakiwa wanajua kusoma na kuandika hivyo kuondoa changamoto hiyo wafikapo darasa la saba.

Aidha, Merisela amesema wadhibiti ubora wamepewa mafunzo katika maeneo ya Udhibiti wa shule, uchambuzi wa mtaala, Muhtasari, Miongozo ya kufundishia KKK, umahiri wa kusoma, kuandika na kuhesabu.

Maeneo mengine ni pamoja na maandalizi ya ufundishaji upimaji unaozingatia umahiri na kuandaa zana za ufuatiliaji wa utekelezaji wa mtaala wa darasa la kwanza na la pili

Baraza Kuu CUF 'lawatumbua' Profesa Lipumba na Sakaya
Rubby Akimbilia EFM,Ni Baada Ya Kutoafikiana Malipo Ya Matamasha Ya Fiesta Yanayoendelea Kwa Sasa