Shirika la la Umeme Tanzania (Tanesco) limeainisha jitihada za muda mfupi na za muda wa kati kukabili changamoto ya upungufu wa umeme nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Novemba 28, 2022 imesema kuwa jitihada za muda mfupi zilizofanyika ili kuingiza jumla ya megawati 90 ni pamoja na kukamilisha matengenezo ya mtambo mmoja wa LM6000 katika kituo cha Ubungo namba III.
Taarifa imeeleza kuwa, tayari huo umeshaanza kuingiza megawati 35 za umeme katika Gridi ya Taifa kuanzia tarehe 25 Novemba kama tulivyoeleza hapo awali, matengenezo ya mtambo mmoja wa kituo cha Kidatu yapo katika hatua za mwisho kukamilika.
- Picha: Waziri Mkuu kassim Majaliwa akikagua mradi wa maji Kisarawe
- Makamu wa Rais afikishwa Mahakamani kwa ufisadi
“Na tunatarajia mtambo huu utaanza kuingiza megawati 50 za umeme katika Gridi ya Taifa ifikapo tarehe 30 Novemba kama tulivyoeleza hapo awali,” imeeleza Taarifa.
“Majaribio ya mitambo miwili katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba I yanaendelea na kwa sasa mitambo hii inaingiza jumla ya megawati 65 za umeme katika Gridi ya Taifa. “Na tunategemea hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Desemba 2022, mitambo hii itakuwa inazalisha jumla ya megawati 90 kama tulivyoeleza hapo awali,” imeeleza taarifa.
Hata hivyo Tanesco imeeleza kuwa bado wanaendelea na kazi za matengenezo ya mitambo miwili ya Ubungo namba III na baada ya kukamilika mwishoni mwa Desemba mwaka huu itazalisha megawati 40 za umeme.