kamanda wa polisi kanda maalum Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, amethibitisha kutokea kwa ajali iliyosababisha vifo vya watu watano na majeruhi 10

Kamanda Mambosasa, amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa daladala

Ajali hiyo iliyotokea leo Oktoba 5, 2020, katika eneo la chang’ombe na imehusisha daladala inayofanya safari kati ya Temeke na Muhimbili na Lori la mchanga.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Aboubakar Kunenge, amewataka madereva wa daladala kuzingatia sheria za barabarani ili kupunguza uwezekano wa kutokea kwa ajali

Halikadhalika, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe, amesema chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa daladala ambapo dereva amekimbia na polisi inaendelea kumtafuta.

Naye, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Aminieli Aligaesha amesema wamepokea majeruhi wa ajali iliyohusisha Daladala na Lori katika eneo la Chang’ombe Temeke Dar es Salaam.

Sita wafariki kwa dhoruba Mexico
NEC yavitahadharisha vyama uvunjifu wa sheria za nchi