Usiku wa kuamkia leo, ulimwengu wa hip hop ulipata habari mbaya za kifo cha rapa nguli ambaye ni mwanafamilia wa kundi maarufu na kongwe la Mobb Deep, Albert Johnson maarufu kama Prodigy, ambacho chanzo chake kimewekwa wazi.
Kwa mujibu wa Billboard, rapa huyo aliyekuwa na umri wa miaka 42 alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya ‘sickle cell (seli nundu) na anemia’. Ugonjwa wa seli nundu alikuwa nao tangu alipozaliwa.
-
Prodigy wa ‘MOBB DEEP’ afariki dunia
Watu wa karibu wameeleza kuwa marehemu Prodigy alikuwa amelazwa kwa muda mrefu katika hospitali moja jijini New York, lakini hali ilikuwa mbaya zaidi jana ambapo jitihada za madaktari kuokoa maisha yake zilishindikana.
Mbali na muziki wa hip hop ambao ulimpa umaarufu mkubwa duniani akiwa na rapa mwenzake Havoc ndani ya Mob Deep, Prodigy aliwahi kushiriki filamu kubwa kama Rhyme and Punishment, Da Hip Hop Witch, A Talent for Trouble na Marda Muzik.