Waendesha mashtaka nchini Ufaransa wamesema moto ulioteketeza Kanisa kuu mjini Paris la Notre Dame ulikuwa ajali ya kawaida.
Mkuu wa Idara ya Mashtaka mjini Paris, Remy Heitz amesema hakuna ishara yoyote kuwa tukio hilo la moto uliozuka katika Kanisa la Notre Dome lilikuwa la kupangwa.
Wakati Ufaransa wanahuzunika kufuatia kuharibiwa kwa moja ya alama zake muhimu.
Kwa mujibu wa DW, Rais wa Ufaransa Emanuel Macron ameahidi kulijenga upya Kanisa hilo ambalo linatazamiwa kuwa kivutio muhimu Barani Ulaya.
Hata hivyo Salamu za pole zimeendelea kutolewa kutoka kote duniani ambapo Papa Francis na Malkia, Elizabeth wa Pili wa Uingereza wamekuwa viongozi wa karibuni kabisa kuelezea masikitiko yao kuhusiana na mkasa wa Notre Dame.
Aidha, Waziri wa Utamudini wa Ufaransa amesema baadhi ya vitu muhimu vilivyokuwemo ndani ya Kanisa hilo vimeokolewa ikiwemo mabaki ya taji la miba linaloaminika kuwa alivalishwa Yesu Kristo na sanamu la mtakatifu Louis.