Moto ulizuka katika Kanisa la Synagogue Church of All Nation (SCOAN) nchini Nigeria, wakati waumini wa kanisa hilo wakiendelea na ibada kuomboleza kifo cha mhubiri maarufu, TB Joshua.

Zaidi ya watu 6,000 walikuwa wamekusanyika kanisani hapo Jumatatu usiku, wakati mjane wa TB Joshua, Bi. Evelyn Joshua alipoongoza ibada katika usiku huo wa mwanga wa mishumaa kusherehekea maisha ya mwanzilishi wa kanisa hilo.

Bumbuli: Wananchi vimbeni, “Simba haitufungi tena”

Taarifa rasmi ya Kanisa hilo ilisema chanzo cha moto ni hitilafu ndogo ya umeme.

Taarifa hiyo inaeleza:

“Jumatatu usiku, Julai 5, 2021, kulikuwa na hitilafu ndogo ya umeme katika chumba kimoja cha jengo la Synagogue Church Of All Nations. Tukio hilo lilidhibitiwa ndani ya muda mfupi na hakuna aliyejeruhiwa.

“Katika kipindi hiki cha wiki ya ibada ya kukumbuka maisha ya Nabii TB Joshua, kanisa lilikuwa linafanya kazi kwa ukaribu na vyombo husika vya Serikali ikiwa ni pamoja na Idara ya Zima Moto ya Lagos, ambayo maafisa wake walikuwa kanisani hapo wakati wa tukio.

“Tunamshukuru Mungu kwa kuendelea kutulinda. Tunauhakikishia umma kuwa hakuna sababu za kuwa na taharuki; na huduma ya kusherehekea maisha ya TB Joshua inaendelea kama ilivyopangwa.”

TB Joshua alifariki dunia Juni 5, 2021 ikiwa ni siku chache kabla ya kufikisha umri wa miaka 58.

Anatarajiwa kuzikwa Julai 9, 2021 katika viunga vya kanisa hilo jijini Lagos.

Limewakuta: Ni polisi wazungu waliomvua nguo zote mwanamke mweusi mlemavu
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 7, 2021