Azzorry Gwanda ni mwandishi wa kujitegemea wa kampuni ya Mwananchi Communication Ltd mwenye kituo cha kazi Kibiti- Pwani ambapo anadaiwa kupotea tangu Novemba 21 mpaka leo haijajulikana alipo.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd, Francis Nanai amesema bado hawajapata sababu ya uhakika iliyofanya mwandishi wao Azzory Gwanda kupotea katika mazingira ya kutatanisha ila amesema kuwa inawezekana sababu ikawa uandishi wake wa habari za mauaji yaliyokuwa yanatokea Kibiti.

Leo amezungumza na waandishi wa habari amewaomba kwa kushirikiana na polisi na vyombo vya usalama kuhakikisha mwandishi huyo aliyepotelea Kibiti anapatikana.

“Siwezi kusema sababu za kupotea kwa ndugu yetu Azorry, lakini inawezekana kutokana na ripoti alizokuwa akizifanya kutokana na mauaji yaliyokuwa yakifanyika Kibiti ikawa sababu ya kukamatwa kwake, lakini pengine tukimpata anaweza kutupa mwanga wa sababu za kukamatwa kwake”.

“Tishio lolote kwa mwandishi ni kuingilia uhuru wa habari, tukio la kutekwa kwa huyu mwandishi ni kuingilia uhuru wa vyombo vya habari. Kama kampuni hatujawahi kupata taarifa kama alikuwa anafuatiliwa au aliwahi kutishiwa maisha kutokana na kazi  alizokuwa anazifanya”. Ameongeza.

Aidha Nanai ameongeza kwa kusema kwamba Mwandishi wao Azzory hakuwahi kuripoti kuhusu kutishiwa amani au kufuatiliwa kwa namna yoyote ndiyo maana hawajui sababu ya kuchukuliwa na watu hao ni nini.

.

 

 

Raila Odinga aonywa vikali kujiapisha
Mchoro wa picha ya Yesu waelekea Abu Dhabi