Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha ACT- Wazalendo, Othman Masoud Othman, amesema hakuna uwezekano kwa Zanzibar kupiga hatua yoyote kimaendeleo, iwapo utaratibu wa sasa wa Muungano utaendeadelea kuwepo kwa vile unainyima Zanzibar Mamlaka ya kufanya maamuzi katika masuala yote muhimu ya ustawi wa uchumi na maendeleo yake.
Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameyasema hayo akiwa Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa chama chake akiwa katika mfululizo wa mikutano ya kisiasa Unguja na Pemba.
Amesema, ili Zanzibar iweze kupiga hatua kuna umuhimu inatakiwa iwe na malaka ya kuweza kufanya mamuzi katika masuala yote ya mipango ya maendeleo ikiwemo maamuzi jinsi ya kuendesha kodi zake bila kuingiliwa na mtu yoyote.
“Mambo yote yaliyoingizwa kinyemela katika orodha ya muungano yanayoibana Zanzibar kiuchumi na kimaendeleo lazima yaondolewe na Zanzibar iweze kuwa na mamlaka kamili katika masuala mbali mbali muhimu na kuwepo muungano wenye ridhaa na manufa kwa pande zote,” amesema Othman.
Aidha, amefafanua kuwa “ujanja na ghilba ndani ya Muungano ulipingwa tokea uhai wa muaasisi wa Mungano huo, ambapo kupitia kitabu cha Marehemu Abdu Jumbe Mwinyi ambaye alikuwa rais wa Zanzibar wa awamu ya pili ameeleza kwamba Mzee Karume hakusema na Mwalimu Nyerere katika kipindi cha mwaka mmoja kabla ya kifo chake na sababu ni Karume kudai kwamba hakubaliani na utaratibu wa kuendesha masuala ya muungano tokea wakati huo.”
Makamu huyo wa Kwanza wa Rais amesema, hata katika Utawala wa Rais Karume mwaka 2001, aliunda Kamati ya kuchunguza matatizo na changamoto ya Muungano na Kamati hiyo kutoa mapendekezo yake, lakini kutokana na nia mbaya waliyonayo upande wa pili mapendekezo hayo yalipuuzwa yalipopelekwa na kuwasilishwa Tanzania bara.
Aidha ameongeza kuwa, ripoti hiyo ya Rais Karume ilipendekeza kwamba hata kukiwepo na kuendelea na mfumo wa Muungano wa Serikali mbili, lakini katika utaratibu wa kupitisha sheria kuwepo na chombo cha kushughulikia masuala ya Tanganyika Pekee na kile cha Zanzibar na baadae kile cha Muungano lakini jambo hilo lilipuuzwa na upande wa pili wa washirika wa muungano.
Amewaeleza wafuasi wa chama hicho kwamba hivi sasa hali ilivyo rais wa Jamhuri ya Muungano anavyopatikana kwa mtindo wa ushindi wingi wa kura hakuwezi kuifanya Zanzibar kuwa na sauri na wala rais bhuyo kuweza kuithamini Zanzibar na ndio maana utawala wa Marehemu Magufuli ulidiriki
kutokuchagua hata waziri mmoja kutoka Zanzibar.
Othman amesema, utaratibu bora wa kumpata rais wa Muunga ni lazima sauti za wananchi wa Zanzibar zisikike kupitia mmalaka yao kwa kuwa na uwezo wa kumkata na kumkubali jambo ambaloi hivi sasa halipo kwenye katiba kwa vile anapatikana kwa wingi wa kura tu.
Hata hivyo, amesema kwamba utaratibu wa sasa unavyoendesha muungano ni sawa na ukoloni kwani ukoloni tafsiri yake ni upande mmoja kuamua utakavyo bila kuushauri upande wa pili jambo ambalo ndilo linalofanyika sasa kwenye muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa mambo mengi hayanaridhaa za wananchi.
Alitoa mfano wa uendeshaji wa bandari, kwamba ijapokua sio suala la muungano kwenye orodha ya mambo yaliyoingizwa kinyemela lakini suala hilo mtindo wake limekuwa likiendeshwa kuibana Zanzibar jambo linaloinyima fursa ya kusonga mbele kwa kukosa mamlaka yake.
Katika kuleta maendeleo ya kweli amesema ni lazima kujenga misingi imara ya kupatikana viongozi kwa mfumo wa kura za uwazi ambao utamfanya kiongozi huo kuthamini na kuwajibika kwa wananchi wote waliomchagua kupitia kura halali za ushindi.
Akizungunzia suala la uwajibikaji wa Viongozi , wizi na ubadhirifu wa mali ya umma Mhe. Othman amesema kwamba viongozi walioingia madarakani kwa njia ya wizi wa kura hawezezi kuwatumikia wananchi na taifa likaweza kusonga mbele kwani nia yao ni madaraka na sio kuwajibika kuwatumikia watu.
Aidha, amewaeleza wafuasi hao kwamba wakati umefika kwa wananchi wote wa Zanzibar kukiunga mkono chama cha ACT Wazalendo ili kiweze kujenga misingi ya kupatikana uongozi kupitia kura halali na wananchi waweze kuwajibisha viongozi hao na wao kuwajibika ipasavyo kwa wananchi.
Naye Mkurugenzi wa Organizesheni na wanachama wa Chama hicho Omar Ali Shehe amesema kwamba wananchi waliathirika mali zao vikiwemo vipando, mashamba na nyumba kupisha ujenzi wa barabara na uwanja wa ndege hadi leo wengi wao hawajalipwa fidia wa waliolipwa wamepewa fedha pungufu
jambo ambalo ni dhulima kwa wananchi.