Jina la Ibrahimu Ajibu lilikuwa miongoni mwa wachezaji wazawa waliojadiliwa katika moja ya vikao vya kamati vya usajili wa Yanga, lakini kamati hiyo imeeleza sababu za kutoafikiana juu ya usajili huo.

Mmoja wa vigogo wa kamati ya usajili ya Yanga aliyeomba hifadhi ya jina amesema baada ya jina la Ajibu kupelekwa mezani kwao, hawakutaka kupepesa macho.

“Ni kweli baadhi yetu walimpendekeza, lakini wengi tulimkataa kwa sababu,” alisema kigogo huyo wa usajili wa Yanga aliyeomba hifadhi ya jina.

“Ajibu sio mchezaji mbaya, lakini inaonekana ameridhika na hatua aliyopo, hivyo alipopendekezwa arudi Yanga, fasta kuna baadhi ya wajumbe walimkataa pale pale bila kupepesa macho,”

“Watu lazima wajue hili, kuna maisha ya kesho kuna namna ambavyo Ajibu aliondoka hapa wengi walikasirishwa hasa ukizingatia klabu, wanachama na mashabiki walimpa heshima kubwa hadi kuwa nahodha lakini alirudi klabu anayoipenda, ni vyema akabaki huko au kwenda klabu zingine zitakazoona anafaa.

“Yanga tutasajili wachezaji bora msimu ujao.” amesema mjumbe huyo.

Kakolanya kusalia Simba
Wamangituka alikana jina lake