Wakati Mbunge wa jimbo la Ushetu, Emanuel Peter Cherehani akiihoji juu ya mkakati wa kupeleka umeme wa uhakika katika halmashauri za Ushetu, Msalala, na Kahama, Serikali imesema Shirika la umeme – TANESCO, lina mpango wa kujenga kituo kidogo cha umeme Wilayani shetu ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme.
Cherehani alitoa hoja hiyo hii leo Novemba 2, 2023 Bungeni jijini Dodoma ambapo Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko alisema TANESCO pia itaongeza njia nyingine za umeme kutokea kituo hicho kwenda Ushetu, Msalala, na Kahama.
Amesema, ujenzi wa mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 12 na mradi unategemewa kukamilika Mwaka wa Fedha 2024/2025.