Rais wa Zanzibar Dr. Hussein Mwinyi amefanya teuzi tatu hii leo ambapo moja ya teuzi hizo amemteua Mtangazaji na Mwandishi wa Habari wa siku nyingi Tanzania Charles Hilary ambae amekua akifanya kazi AzamTV kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano – IKULU Zanzibar.
Rais Mwinyi amemteua pia Yusuph Majid kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) na amemteua Idrissa Haji kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uhaulishaji Ardhi Zanzibar.