Aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu ya Wanawake Simba ‘Simba Queens’ Charles Lukula amepata ofa ya kuifundisha timu ya Taifa ya Wanawake ya Uganda ‘The Crested’.

Kocha huyo amesema baada ya kumaliza mkataba wake na Simba SC amepokea ofa nyingi nchini na Uganda ikiwemo timu ya taifa ya wanawake ya Uganda.

“Tangu niondoke Tanzania nimepokea ofa nyingi baadhi zinatoka kwenye timu za Ligi Kuu za wanaume na wanawake pamoja na hii ya Uganda ninachoangalia ni maslahi yangu, naifikiria zaidi timu yangu ya taifa ya wanawake,” amesema Lukula.

Kocha huyo amesema Wakala wake Mujibu Kasule anaendelea kufanya mazungumzo na klabu mbali mbali pamoja na timu hiyo ya taifa.

“Mimi siruhusiwi kuzungumza nazo, Wakala wangu ndio anafanya mazungumzo tukikamilisha mipango yote nitawafahamisha ninapo kwenda,” amesema Lukula.

Aidha amesema anaushukuru Uongozi wa Klabu ya Simba kwa kumuamini na kumpa nafasi yakufundisha timu yao ya wanawake na amejifunza mengi.

Amesema Ligi Kuu ya Wanawake ya Tanzania ina ushindani mkubwa ukilinganisha na nchi nyigine hususaani za Afrika mashariki ambazo zinapaswa kujifunza kwao.

“Soka la Tanzania kwa wanawake imepiga hatua kubwa sana, timu nyingi zina wachezaji a kimataifa na wanaleta ushindani kwa wachezaji wazawa, tanzania imepiga hatua kubwa sana. amesema Lukula.

Aidha amesema wameukosa kutetea ubingwa wao msimu huu kutokana mapungufu kwa baadhi ya maeneo ikiwemo eneo la golikipa.

“Mimi ningepata ubingwa isipokuwa makipa wangu ndio wameniangusha na timu yangu ilikuwa imefanya vizuri kwenye michezo yake yote, ni jambo la kuliangalia,” amesema Lukula

Fursa kimaendeleo: Mbunge ataka vikundi imara vya Bodaboda
Bellingham aweka rekodi nzito England