Chama Cha Sanaa Mbeya – CHASAMBE, wameiomba Serikali na Jamii kuwatambua na kuwapa fursa mbalimbali Ikiwemo Kushiriki katika matamasha yanayohamasisha Maendeleo.
Akizungumza kwa niaba ya Wasanii wa Mbeya Mwenyekiti wa CHASAMBE, Farida Ngoyi amesema jamii na Serikali isiwape Wasanii wanaotoka Nje ya Mbeya kipaumbele hasa kwenye Matamasha makubwa kwani kitendo hicho ni kudhoofisha Sanaa ya Mbeya.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amewaondoa hofu na kuwahakikishia Serikali Itawaunga mkono na kwa katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane, yatakayofanyika Mbeya itawapa nafasi ya Kusherehesha na kuonesha vipaji vyao.
Aidha, amewataka kuongeza ubunifu huku akisema, “Sanaa ni nyenzo kubwa inayotumika katika Kuelimisha, Kufundisha na Kuonya hivyo basi itumieni kukemea vitendo vya mmomonyoko wa maadili na Ukatili wa Kijinsia.”
Malisa ameongeza kuwa, “Bila kusahau kutumia Sanaa kuyasema makubwa yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.”
Chasambe Ni chama Chenye wanachama hai 616 chama hiko kina jumping Wasanii wa sanaa zote Wanaopatikana Jijini Mbeya.