Beki wa kati wa Simba SC, Mcameroon, Che Fondoh Malone amegomea mapumziko waliyopewa chini ya Benchi la Ufundi la timu hiyo linaloongozwa na Kocha Mkuu Robert Oliveira Robertinho’ kwa kusema kuwa hana muda wa kupumzika na amepanga kutumia siku nne kwa ajili ya kujifua zaidi.

Beki huyo tayari ameshajihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha Robertinho baada ya kufanikiwa kufanya vizuri huku akitengeneza muunganiko mzuri na baadhi ya mabeki akiwemo Henock Inonga na Kennedy Juma. 

Akizungumza jijini Dar es salaam, Che Malone amesema kuwa, hakuna muda wa kupumzika ni wakati wa kufanya kazi na kujiweka fiti ili watakaporejea kambini asianze kazi upya.

Hakuna likizo hakuna muda wa kupumzika, kila siku ni kazi ili kupata kilele ni rahisi lakini kukaa kileleni ndio ngumu zaidi, jambo la kufanya kuendelea kuwa na nguvu na ukifanyia kazi utafika,” amesema beki huyo ambaye anatumia siku nne za mapumziko kuendelea kujifua.

“Nahitaji kuonyesha kiwango kizuri na bora ili kusaidia timu yangu kuweza kufikia malengo ambayo tumejiwekea, ligi imekuwa ngumu kutokana na ushindani uliopo hivyo nahitaji kuwa bora zaidi kuweza kwenda sawa na hali ilivyo,” amesema Che Malone.

Mashujaa FC kutafuta makali zaidi Burundi
Waandamana kupinga idadi kubwa ya Watalii