Kiongozi Mkuu wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya, Wafula Chebukati amewaondoa viongozi wa ngazi za juu waliosimamia uchaguzi uliofutwa na kuteua tume mpya ili kusimamia uchaguzi wa marudio.

Chebukati amewatimua viongozi waliotajwa na NASA kuwa hawana imani nao, ni pamoja na CEO Ezra Chiloba na msaidizi wake Betty Nyabuto, Mkurugenzi mtendaji tume ya upigaji kura na Uchaguzi, Immaculate Kasait, meneja  Junior Mwaura pamoja na aliyekuwa kiongozi Mkuu kitengo cha Mawasiliano na Teknolojia  James Muhati.

Kupitia utenguzi huo Chebukati ameteua viongozi wengine sita kuratibu marudio ya uchaguzi nchini Kenya yatakayofanyika Octoba, 17 mwaka huu.

Viongozi hao wapya wamepewa mkataba wa miaka 3 na miongoni mwao yupo Mkuu mpya wa ICT, Bw. Albert Gogo.

”Kwa uwezo wangu kama Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa Urais kwa kuzingatia Kifungu cha Sheria cha mwaka 2011, nimewateua watu wafuatao kwa lengo la kusimamia marudio ya uchaguzi mkuu wa Urais utakaofanyika Oktoba 17, 2017”.Amesema Chebukati

 

RC Tabora aagiza kukamatwa kwa viongozi wa ushirika
Simba na Yanga sasa kucheza Azam Complex