Moja kati ya vitu vilivyotawala mitandao ya kijamii jana Afrika Mashariki, ni picha iliyosambaa ikionesha rais wa Uganda Yoweri Museveni akiwa amesimamisha msafara wake akipiga simu ya dharura pembeni ya barabara akiwa amekaa kwenye kiti kama yuko nyumbani kwake.

Watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii walifanya ubunifu wao kuweka ucheshi katika picha hiyo ambayo awali haikuwa na maelezo ya kutosha.

Kwenye mtandao wa Twitter wameendelea kukuza trend iliyopewa jina la #M7Challenge wakiweka picha na video zinazoigiza tukio hilo.

Mchekeshaji wa Kenya, Eric Omondi ni mmoja kati ya waliozua ucheshi kwa kumuiga Rais Museveni, lakini yeye alikaa katikati ya barabara ya Kileleshwa na kusababisha msongamano wa magari.

Baadhi ya vituko vingine vilivyowekwa;

President @KagutaMuseveni photo in Isingiro now sparks a new trending #M7Challenge pic.twitter.com/RplC3g4siL


Hata hivyo, kipande cha video kilichotolewa na Kurugenzi ya Ikulu ya Uganda kilionesha kuwa Museveni alisubiri katika eneo hilo na kuzungumza na wanakijini waliokuwa wakiishi katika eneo hilo, kabla ya kupanda chopa iliyomfuata mahali hapo. Haikuwekwa wazi moja kwa moja sababu ya kusimama katika eneo hilo linaloonekana liko mbali na mji.

Museveni na wanchi wake

Mohamed Mustapha na Wenzake Kortini kwa Kuiletea Serikali Hasara ya Bil.15
Magufuli Aanika Rushwa za JK. Chadema yawekewa Ulinzi Kila Kona DOdoma