Timu za Chelsea na Arsenal zinatarajia kuonyeshana ubabe katika mchezo wa fainali ya kombe la FA unaotarajiwa kuchezwa hii leo katika dimba la Wembley jijini London.

Chelsea ambao ni mabingwa wa EPL wametamba kutwaa ndoo hiyo ya FA na kuweka historia ya kujikusanyia vikombe viwili ndani ya msimu mmoja.

“Ninataka kuweka historia katika ligi kuu ya Uingereza kwa kutwaa mataji mawili ndani msimu mmoja, timu yangu iko vizuri na wachezaji wana ari kubwa ya mchezo hivyo ushindi kwetu ni uhakika,”amesema Kocha wa timu hiyo, Antonio Konte.

Kwa upande wake kocha wa Arsenal, Arsenal Wenger amesema kuwa pamoja na kumaliza wakiwa katika nafasi ya tano katika ligi hiyo, bado wanayo nafasi kubwa  ya kutwaa kombe la FA kwani ndilo pekee wanalopigania.

“Tunataka tuweke heshima ya kutwaa kombe hili, kwani kumaliza ligi tukiwa nafasi ya tano si kigezo cha kushindwa kuchukua kombe hili, wachezaji wangu wako vizuri na wana ari na shauku ya kutwaa ubingwa wa FA, amesema Arsenal Wenger.

Wawili wauawa wakizuia udhalilishaji dhidi ya wanawake wa Kiislam
Marekani kuweka kifaa maalum cha kutungua makombora