Michuano ya klabu bingwa barani Ulaya inatarajia kuendeelea usiku wa leo huku michezo minne ikitarajiwa kupigwa katika viwanja tofauti.

Manchester United watakuwa nyumbani katika dimba la Old trafford kuwakaribisha Benfica, United wakipata ushindi leo watakuwa wamefuzu kwenda katika hatua ya 16 bora lakini hiyo ni iwapo CSKA Moscow watafungwa au kutoka sare na FC Basel

As Roma wanaikaribisha Chelsea hii leo wakiwa na kumbukumbu ya kuwafunga mabao 3-1 mwaka 2008 katika uwanja wao wa Stadio Olimpico na habari njema kwa Chelsea ni kwamba leo Ngolo Kante anarejea huku katika kundi lao mchezo mwingine utakuwa kati ya Atletico Madrid dhidi ya Qarabag FK utakaopigwa kesho.

Katika mchezo mwingine Celtic watakuwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Celtic Park kuwakaribisha Bayern Munich.

Video: JB kuachana na uigizaji wa filamu
LIVE: Rais Magufuli akihutubia katika uzinduzi wa kiwanda cha dawa Mwanza