Klabu ya Chelsea imewapa taarifa wachezaji wake walio nje ya Uingereza kurejea klabuni mwishoni mwa juma hili, tayari kwa kuanza mazoezi ya pamoja kabla ya kuendelea kwa msimu wa ligi kuu ya England.

Ligi ya nchi hiyo ambayo ni maarufu duniani, ilisimama kupisha vita dhidi ya janga la maambukizi ya Corona, ambalo linaendelea kuzitesa baadhi ya nchi.

Uongozi wa klabu hiyo ya jijini London, umetuma taarifa hiyo kwa wachezaji wake, kutokana na uwezekano wa kurejea kwa michezo ya igi kuu ya England kuwa amkubwa siku za usoni.

Tayari wachezaji wa klabu za Arsenal na West Ham wameshaanza mazoezi ya pamoja, na klabu hizo zimekua klabu pekee zilizoanza utaratibu huo wa kujiandaa na michezo iliyosalia.

Hata hivyo kuna uwezekano mdogo wa ligi kuu Uingereza kuhairishwa kama ligi nyengine haswa kutokana na hasara inayotajwa kufikia zaidi ya paundi milioni 800 kama ligi hiyo ikihairishwa. Hadi ligi kuu ya England inaahirishwa, Liverpool walikua kileleni kwa kufikisha alama 82, wakifuatiwa na Manchester City [Alama 57], Leicester City inashika nafasi ya tatu [Alama 53] huku Chelsea ikiwa nafasi ya nne [Alama 48].  

Kim Jong-un aonekana hadharani, afanya hili kukiwa na tetesi kuwa amefariki
Meddie Kagere apendekeza ubora wachezaji wa kigeni