Klabu ya Chelsea haitafanya usajili wa mkwanja mrefu mwezi Januari 2024 na itakuwa makini kusaka wachezaji wapya, imeelezwa.
Chelsea imepanga kusajili wachezaji wawili au watatu dirisha la usajili la mwezi Januari 2024, kama sehemu ya kuimarisha kikosi cha Mauricio Pochettino, kwa mujibu wa The Telegraph.
Chelsea pia imapanga kuuza baadhi ya wachezaji endapo itapata ofa nzuri mwezi Januari 2024, ambazo itatumia kusajili Mshambuliaji mpya na beki.
Wachezaji ambao wanatarajiwa kuondoka Januari 2024 ni Trevoh Chalobah anayehusishwa na Bayern Munich, huku Armando Broja, lan Maatsen, Malang Sarr na Conor Gallagher wakitajwa.
Sera mpya ya Chelsea ni jaribio la kuzuia timu ya Pochettino kuwa na wachezaji wengi ambao hawapati nafasi kama ilivyokuwa msimu uliopita.
Kocha wa zamani wa Chelsea, Graham Potter kikosi chake kilisheheni wachezani 31 waliokuwa wakipigania nafasi ya kudumu katika kikosi chake.
Timu hiyo kutoka Jiji la London ilianza kusajili wachezaji wanne wapya ingawa wachezaji l6 wa kikosi cha msimu uliopita waliondoka wakiwemo Mason Mount, Edouard Mendy, Kalidou Koulibaly, N’Golo Kante, Mateo Kovacic na Kai Havertz.
Taarifa zimeripoti huenda Chelsea ikajaribu bahati kwa Victor Osimhen mwenye thamani ya Pauni 100 milioni, ili kutatua mapungufu katika safu ya ushambuliaji.
Mshambuliaji huyo wa SSC Napoli alikuwa hatari msimu uliopita kwani aliisaidia klabu hiyo kubeba ubingwa kwa mara ya kwanza tangu miaka 33.