Kiungo wa kati wa klabu ya Chelsea N’Golo Kante hataweza kucheza kwa wiki tatu baada ya kuumia misuli ya paja akicheza katika timu ya taifa ya Ufaransa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 aliondoka uwanjani akiwa anachechemea baada ya mechi ambayo Ufaransa waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bulgaria wikendi iliyopita na sasa hataweza kucheza hadi mwezi ujao.

Antonio Conte amesema kutokana na kukosekana kwa Kante huenda akahitajika kuchezesha baadhi ya mabeki kama viung wa kati huku pia akitegemea mshambuliaji Alvaro Morata kuwa sawa kucheza dhidi ya Roma Jumatano katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Kocha huyo amesema kwamba mchezaji N’golo Kante atahitaji kupigwa picha ya uchuguzi wa kidaktari mguuni na kuchunguzwa zaidi.

Wakati huo huo kiungo wa kati mwenzake Danny Drinkwater anapiga hatua vyema katika kuuguza jeraha la misuli ya sehemu ya chini ya miguu lakini bado hayuko tayari kuichezea Chelsea mechi yake ya kwanza.

 

 

 

Video: Mpina aagiza kuuzwa kwa ngo'mbe waliokamatwa
Upande wa mashtaka wapewa siku 14