Imeelezwa kuwa Klabu ya Chelsea inajipanga kuanza upya mazungumzo na Uongozi wa Brighton kwa ajili ya kumsajili kiungo, Moises Caicedo.
The Blues ipo kwenye mchakato wa kunasa saini ya kiungo mpya tangu dirisha la majira haya ya kiangazi huko Ulaya lilipofunguliwa.
Kwa mujibu wa mkali wa masuala ya usajili, Fabrizio Romano, wataanzisha mazungumzo na moja ya klabu zenye kiungo wanayemtaka ndani ya saa 24 au 48 zijazo.
Chelsea imeripotiwa ipo tayari kulipa hadi Pauni 80 milioni kunasa saini ya kiungo huyo, lakini Brighton huenda wakahitaji mkwanja mrefu zaidi.
Makubaliano binafsi ya mchezaji tayari yameshafikiwa mwafaka na Caicedo yupo tayari kwenda kukipiga Stamford Bridge.
Arsenal na Manchester United nazo zilikuwa kwenye mchakato wa kunasa saini ya kiungo huyo kwenye dirisha hili, lakini Chelsea wanaonekana kuwa siriazi zaidi.
Arsenal awali walionyesha kuhitaji saini yake, kabla ya Kocha Mikel Arteta kuweka nguvu zaidi kwenye usajili wa kiungo Declan Rice, ambaye amemwekea mezani Pauni 105 milioni.
Man United wanadaiwa kugeuzia mpango wao kwa Caicedo baada ya kukwama kwa Mason Mount wa Chelsea.
Man United imepeleka ofa tatu huko Chelsea, ikiwamo ya Pauni 55 milioni, lakini zote zimekataliwa. Hapo kocha wa Man United, Erik ten Hag anaamini atawapiku Chelsea kwenye usajili wa Caicedo.