Klabu ya Chelsea inafuatilia hali ya Victor Osimhen katika klabu ya SSC Napoli baada ya wakala wa mshambuliaji huyo kuwatishia mabingwa hao wa Italia atawafikisha katika vyombo vya sheria.
The Blues hao kwa muda mrefu wamekuwa wakimfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria, ambaye aliiongoza SSC Napoli kutwaa taji lao la kwanza la Serie A katika kipindi cha miaka 33 msimu uliopita.
Mwezi Februari, mwaka huu Osimhen ndiye alikuwa mshambuliaji wa kwanza kuwaniwa na Chelsea kabla ya dirisha la usajili la majira ya joto.
Lakini huku mshambuliaji huyo akionekana kukaribia makubaliano ya mkataba mpya huko SSC Napoli, walibadilisha vipaumbele mahali pengine Chelsea ilimaliza kusajili wachezaji 12 kabla ya msimu wa 2023/24 badala yake na kumwona Osimhen kama shabaha zaidi ya kufikiwa msimu wa joto mwakani.
Hali sasa inatishia kubadilika, kwani wakala wa Osimhen, Roberto Calenda, amethibitisha wanafikiria kuchukua hatua za kisheria dhidi ya SSC Napoli baada ya klabu hiyo kutuma video inayomdharirisha mshambuliaji huyo kwenye TikTok.
Video hiyo imeondolewa, lakini Osimhen amekasirishwa na namna klabu hiyo ilivyomchukulia.
Calenda alisema: “Kilichotokea katika akaunti rasmi ya SSC Napoli kwenye ukurasa wa TikTok hakikubaliki. Video ya kumdhihaki Victor iliwekwa wazi kwanza na baadae ikafutwa.
“Jambo kubwa ambalo husababisha madhara makubwa kwa mchezaji. Tunahifadhi haki ya kuchukua hatua za kisheria na mpango wowote muhimu wa kumlinda Victor.”
Mapema Jumatano, iliripotiwa kuwa mazungumzo kati ya Osimhen na SSC Napoli juu ya mkataba mpya yalisitishwa.
Mkataba wa Osimhen kwa sasa unaendelea hadi 2025, wakati mkataba wowote mpya huko SSC Napoli ulitarajiwa kuja na kifungu cha kutolewa kwa pauni milioni 150.
Hitaji la Chelsea la kutaka mshambuliaji mpya nyota limekuwa kubwa zaidi kufuatia kuanza kwa msimu vibaya.
The Blues wameshinda mchezo mmoja tu kati ya sita ya mwanzo za Ligi Kuu England, wakifunga mabao matano pekee.