Kocha Mkuu wa Chelsea Mauricio Pochettino anaendelea kukijenga kikosi chake, huku taarifa zikieleza kuwa amejipanga kumsajili Axel Disasi akitokea AS Monaco ya Ufaransa.

Chelsea inajiandaa kumsajili beki huyo kutoka Ufaransa mwenye umri wa miaka 25, kwa ada ya Pauni Milioni 38, ili kuchukuwa nafasi ya beki Wesley Fofana ambaye ni majeruhi kwa sasa.

Tayari Chelsea inaripotiwa kukubali kutoa kiasi hicho cha fedha baada ya kukamilisha mazungumzo na Uongozi wa AS Monaco, ambao umeonesha kufurahishwa na biashara hiyo.

Disasi alisajiliwa AS Monaco mwaka 2020 akitokea Reims, na mara kwa mara alikuwa anahusishwa na usajili kutoka kwenye klabu zinazoshiriki Ligi Kuu ya England ‘Premier League’.

Klabu ya Manchester United ni sehemu ya klabu zilizotajwa kuwahi kuhusishwa na usajili wa Beki huyo, ambaye sasa atafanya kazi chini ya Kocha Mauricio Pochettino.

Disasi atajiunga na wachezaji waliosajiliwa Chelsea katika kipindi hiki ambao ni Christopher Nkunku, Nicolas Jackson pamoja na Angelo Gabriel.

Rais ZFF: Dhamira yangu ina maono ya mbali
Tanzania, Algeria kuimarisha Diplomasia ya Uchumi