Baada ya kumtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari, uongozi wa klabu ya Chelsea umeahidi kumtengea sehemu maalum meneja wao mpya kutoka nchini Italia, Maurizio Sarri ambayo ataitumia kwa ajili ya kuvutia sigara.
Meneja huyo mwenye umri wa miaka 59, huvuta sigara 80 kwa siku, jambo ambalo linadhihirisha wakati wote hulazimika kuburudika na kilevi hicho (Akiwa mazoezini, na wakati wa michezo ya ligi).
Uongozi wa Chelsea umenadi kufanya hivyo, baada ya kuulizwa na waandishi wa habari juu ya tabia ya meneja huyo ya uvutaji wa sigara kupita kiasi, huku sheria za England zikikataza uvutaji wa sigara hadharani.
The Bules wamesema kabla ya kufikia makubaliano ya kumuajiri Sarri, walijua starehe yake ya uvutaji wa sigara, na wanamini ni vigumu kumshauri kuacha, hivyo wameona ni jambo la busara kumtengea chumba maaluma mbacho atakua akikitumia kwa ajili hiyo.
Hata hivyo uongozi wa Chelsea umetanabaisha kuwa, chumba hicho cha uvutaji kutatengwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge pamoja na eneo la uwanja wa mazoezi.
Alipokua SSC Napoli, meneja huyo alipewa ruhusa ya kuvuta sigara akiwa katika benchi la ufundi wakati wa mapumziko, na alifanya hivyo mara kwa mara kutokana na hitaji la uvutaji wa sigara kwa wakati husika.
Meneja huyo amepewa jukumu zito la kuhakikisha anairejesha Chelsea katika kiwango cha ushindani na kurejesha heshima ya kutwaa ubingwa wa England msimu ujao, baada ya ubingwa wa EPL kuwaponyoka na kwenda Etihad Stadium yalipo makao makuu ya Man city.
Kazi nyingine kwa Sarri itakua ni kuhakikisha The Blues wanapambana vizuri kwenye michuano ya Europa League na kufikia lengo la kutwaa ubingwa.