Klabu ya Chelsea imeendelea kufanya vyema EPL baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Aston Villa. Nicholas Jackson alikuwa wa kwanza kufungua akauti ya mabao kwa bao lake la mapema dakika ya 7 ya mchezo .Enzo Fernandez aliandika bao la pili dakika ya 36 na kuufanya mchezo kwenda mapumziko Chelsea wakiwa mbele kwa mabao 2-0.
Cole Palmer alifunga bao la tatu dakika ya 83 na kuwafanya Chelsea kufikisha alama 25 katika michezo 13 nyuma ya Arsenal aliye nafasi ya pili kwenye msimamo wa EPL.
LIVERPOOL YASALIA KILELENI
Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester City umewafanya Liverpool kusalia kileleni kwa tofauti ya alama 9 dhidi ya Chelsea na Arsenal.Liverpool wana alama 34 kwenye msimamo wa ligi huku Chelsea nafasi ya tatu na Arsenal nafasi ya 2 wakiwa na alama 25 kila mmoja.
Katika mchezo wa EPL dhidi ya Manchester City Cody Gakpo alikuwa wa kwanza kufungua akaunti ya mabao kwa bao la dakika ya 12 na Mohammed Salah kukamilisha ushindi huo kwa bao la mkwaju wa penati dakika ya 78.
Kwa sasa Manchester City ni kama imepoteza muelekeo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kukusanya alama 23 pekee katika michezo 13 waliyocheza.City wameshinda michezo 7 sare 2 na kupoteza michezo minne mfululizo dhidi ya Bournemouth 2-1,Brighton 2