Klabu za Chelsea na Manchester United zinafuatilia kwa karibu maendeleo ya beki wa Paris Saint-Germain Marquinhos ili kujaribu kumsajili dirisha dogo la Januari.

Beki huyo kijana wa Brazil alisaini mkataba mpya mwaka jana licha ya ofa za Chelsea na Manchester United kukataliwa, lakini sasa ameanza kuumizwa na benchi analosugua PSG akiwa ameanza katika mechi saba tu msimu huu.

PSG inaonekana haitakuwa tayari kufanya biashara mwezi Januari, lakini akiongea na gazeti la Journal du Dimanche, Marquinhos mwenye umri wa miaka 21, alikiri kuwa uvumilivu unaanza kumshinda.

Alisema: “Kama ilivyo kwa mtu yeyote yule, siku zote nimekuwa nikiwaza kuwa chaguo la kwanza. Lakini unapaswa kuheshimu maamuzi ya kocha.

“Nitaendelea kufanya kazi kwa bidii kupigania nafasi yangu. Ni ukweli kuwa kuna wakati unahitaji zaidi. Hatuwezi kutumika muda wote kama wachezaji wa akiba.”

Mbwana Samatta Kwenda Nigeria Na Katibu Wa TFF
Marko Grujic Yu Njiani Kuelekea Anfield