Chelsea wamefikia makubaliano na Barcelona kumsajili winga Pedro kwa pauni milioni 21.

Mchezaji huyo, mwenye umri wa miaka 28, ambaye alikuwa akisakwa na Manchester United, anasafiri kwenda London kukamilisha uhamisho wake.

Pedro amepachika mabao 99 katika mechi 326 tangu alipoanza kucheza mwaka 2008.

Atakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Chelsea ndani ya wiki moja, kufuatia kuwasili kwa beki wa kimataifa wa Ghana Abdul Baba Rahman.

Serikali Yampiga 'Marufuku’ Lowassa Kutumia Uwanja Wa Taifa
Purukushani Za Usajili Barani Ulaya