Mabingwa wa soka nchini England, Chelsea wameanza mikakati ya kutaka kumsajili beki kutoka nchini Ujerumani na klabu ya Borussia Dortmund, Mats Hummels.

Kwa mujibu wa gazeti la Bild la nchini Ujerumani, The Blues wameanza mipango hiyo kwa kumbembeleza baba mzazi wa beki huyo, ili kulainisha mambo kabla ya kumfikia muhusika.

Hummels, mwenye umri wa miaka 27, thamani yake ni paund million 27 na hana wakala ambaye ataweza kuingilai kati kuhusu dili lake la kusajiliwa mwishoni mwa msimu huu.

Meneja anaetajwa huenda akapewa jukumu la kukinoa kikosi Chelsea mara baada ya fainali za mataifa ya barani Ulaya, Antonio Conte amekua katika harakati za kutaka kuona ushindani unakuwepo katika kikosi hicho cha magharibi mwa jijini London.

Conte, anatajwa kuwa na hamu ya kutaka kuleta mapinduzi ya ushiriki wenye ushindani katika michuano kadhaa ambayo Chelsea watashiriki msimu ujao wa ligi, ili aonyehe tofauti kati yake na mameneja waliomtangulia Jose Mourinho na Guus Hidink.

Man City Waanza Kutii Maagizo Ya Guardiola
Mkwasa Awaita Watanzania Uwanja Wa Taifa