Mabingwa wa soka nchini England, Chelsea wameanza kufanya mazungumzo ya usajili wa mlinda mlango kutoka Bosnia na Herzegovina Asmir Begovic.

Chelsea wameamua kufanya hivyo kwa lengo la kumsaka mbadala wa Petr Cech ambaye jana jioni aliwaaga rasmi baada ya kujiunga na Arsenal yenye maskani yake huko kaskazini mwa jijini London.

Mazungumzo baina ya pande hizo mbili yameripotiwa kuanza kufanyika saa chache baada ya uthibitisho wa Petr Cech kujiunga na The Gunners. Viongozi wa The Blues wana matumaini makubwa ya kufanikiwa kumsajili mlanda mlango huyo wa klabu ya Stoke City.

Chagizo la kusajiliwa kwa Begovic, limekua likipewa kipaumbele na meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho kutokana na kuamini kwamba atakua chaguo sahihi la kumsaidia mlinda mlango wake namba moja kutoka nchini Ubelgiji, Thibaut Courtois.

Hata hivyo taarifa zinaeleza kwamba uongozi wa klabu ya Stoke City umeweka msisitizo wa kumuachia Begovic kwa ada ya uhamisho wa paund million 10 na tayari wameshaikataa ofa ya paund million 6 iliyowasilishwa na Chelsea.

Mafuta Bei Juu, Walioyaficha Kuanza Kuadhibiwa
Chile Yaitendea Haki Ardhi Ya Nyumbani, Yazisubiri Argentina Na Paraguay