Klabu ya Chelsea imeingia kwenye orodha ya klabu za England zilizofikisha zaidi ya alama 2000, tangu kuanzishwa kwa ligi kuu ya nchi hiyo Februari 20 mwaka 1992.

Chelsea wamefikisha alama 2000, baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya England msimu huu dhidi ya Brighton & Hove Albion, juzi jumatatu.

Hata hivyo klabu hiyo ya jijini London imetanguliwa na Manchester United wanaoongoza kwenye orodha ya klabu zilizofikisha zaidi ya alama 2000, ikifuatiwa na Arsenal na The Blues wanashika nafasi ya tatu.

Lakini katika orodha hiyo klabu hizo tatu ndizo zimefikisha alama 2000 na zaidi, na zinazofuatia bado zipo chini ya alama hizo.

Orodha ya klabu 20 ambazo zina alama nyingi zaidi tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu ya England miaka 28 iliyopita.

  1. Manchester United – 2,231
  2. Arsenal – 2,014
  3. Chelsea – 2,000
  4. Liverpool – 1,951
  5. Tottenham Hotspur – 1,654
  6. Everton – 1,479
  7. Manchester City – 1,450
  8. Newcastle United – 1,319
  9. Aston Villa – 1,258
  10. West Ham United – 1,137
  11. Southampton – 980
  12. Blackburn Rovers – 970
  13. Leeds United – 692
  14. Leicester City – 672
  15. Middlesbrough – 661
  16. Sunderland – 618
  17. Fulham – 612
  18. Bolton Wanderers – 575
  19. Crystal Palace – 475
  20. West Bromwich Albion – 464

Picha: Aubameyang amaliza ukimya kwa vitendo
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 16, 2020