Manchester United wamesusia kutoa mkwanja mrefu ili kumsajili Mason Mount wa Chelsea, huku ikielezwa klabu hiyo ipo tayari kutoa Pauni milioni 40.
Meneja wa United, Erik ten Hag anaamini Mount mwenye umri wa miaka 24, anaweza kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kama akimsajili,
Hata hivyo haoni haja ya mabosi wake kumwaga pesa nyingi ikizingatiwa kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza amebakiza mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake.
United haioni sawa kutoa Pauni milioni 70 dau ambalo wanalitaka Chelsea ili kumuachia staa huyo.
United huenda ikatoa ofa nyingine kwa kiungo huyo mshambuliaji lakini wanazingatia bajeti yao ambayo wameipanga kwenye usajili huu wa majira ya joto.
Kwa sababu hiyo hiyo inaonekana kuwa kuna uwezekano wakaachana na dili la kumsajili mshambuliaji Harry Kane mwenye umri wa miaka 29, kutoka Tottenham kwa kuwa thamani yake inayotajwa kuwa ni Pauni millioni 100.