Klabu ya Arsenal imefikia makubaliano binafsi na kiungo wa Brighton, Moises Caicedo lakini itapata upinzani kutoka kwa Chelsea.
Taarifa zinaeleza kuwa Caicedo anatamani kucheza michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya huku Arsenal ikipewa nafasi kubwa ya kunasa saini yake.
Kwa mujibu wa taarifa Chelsea imepania kutoa mkwanja mrefu na kuipiku Arsenal, ingawa haitashiriki michuano ya Ulaya msimu ujao.
Liverpool ilionyesha nia ya kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21, lakini sio chaguo la kwanza la kocha Jurgen Klopp kwasasa.
Brighton inatarajia kwamba itamruhusu Caicedo dirisha hili la usajili la kiangazi baada ya Arsenal kushindwa kutoa Pauni 70 milioni katika dirisha dogo la usajili Januari.
Arsenal imepania kuongeza kiungo mwingine atakayeziba pengo la Granit Xhaka anayetarajia kutua Bayer Leverkusen kwa mujibu wa ripoti.
Wakati huohuo Arsenal bado haijakata tamaa ya kunasa saini ya kiungo wa West Ham, Declan Rice baada ya kumfukuzia kwa muda mrefu.
kwa upande wa Chelsea imeendelea na mipango ya kujenga timu chini ya kocha Mauricio Pochettino aliyeteuliwa hivi karibuni.
Jambo la kwanza kkwa ocha huyo ni kwamba atapunguza baadhi ya wachezaji ambao hawana uhakika wa namba msimu ujao wakiwemo Mateo Kovacic na Mason Mount.