Klabu ya Soka ya Chelsea imejifariji kwa kunyakua kombe la FA baada ya kuitandika Klabu ya Manchester United 1-0 na kujitwalia kombe hilo kongwe nchini Uingereza.
Fainali hiyo ilichezwa katika dimba la Wembley jijini London na kufanya kombe hilo kubaki jijini humo likihama kutoka Emirates hadi Stamford Bridge.
Bao la Chelsea lilipatikana kupitia mkwaju wa penati dakika ya 22, likifungwa na nyota wa Ubeligji, Eden Hazard ambaye aliangushwa na mlinzi, Phil Jones wa Man United kwenye eneo la hatari.
Aidha, kwa ushindi huo Chelsea wameepuka kufuata rekodi ya Newcastle United mwaka 1998 na 1999 ilipofungwa fainali mara mbili mfululizo. Chelsea nayo msimu uliopita ilipoteza mchezo wa fainali dhidi ya Arsenal.
-
Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Misri
-
Guardiola amwaga wino tena Man City
-
West Ham yamnyemelea Manuel Pellegrini
Hata hivyo, Mancheter United wao wameshindwa kufikia rekodi ya Arsenal ya kutwaa taji hilo mara nyingi zaidi ambapo ni mara 13. Baada ya kufungwa wamebaki na ubingwa wao mara 12 huku wakicheza fainali mara 20 sawa na Arsenal.