Klabu ya Chelsea itaamua iwapo itaongeza kasi ya kumsajili, Dusan Vlahovic baada ya mshambuliaji, Christopher Nkunku kuondolewa kikosini kwa muda kufuatia upasuaji wa goti.
Nkunku, aliyesajiliwa kwa Euro Milioni 60 majira ya joto kutoka RB Leipzig, alipata jeraha huko Chicago wakati wa mechi ya mwisho ya kirafiki, Chelsea ikiwakabili Borussia Dortmund wiki iliyopita.
Katika taarifa ya Klabu hiyo ya jijini London imeelezwa kuwa, Nkunku amepatajeraha la goti ambalo litamfanya kuwa nje ya Uwanja kwa muda mrefu.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amefanyiwa upasuaji na sasa ataanza kujiuguza.
Dalili za awali zinaonyesha Nkunku anaweza kukaa nje ya uwanja kwa angalau miezi mitatu, habari ambazo zitakuja karma pigo kubwa kwa kocha mpya, Mauricio Pochettino.
Nkunku alikuwa mmoja wa wachezaji wa Chelsea waliofanya vizuri zaidi katika ziara yao nchini Marekani, akifunga mara tatu, huku Pochettino akijaribu kubadilisha kikosi kilichofunga mabao 38 pekee katika mechi 38 za Ligi Kuu England msimu uliopita.
Vyanzo viliiambia ESPN hitaji la klabu la kuwa na moto zaidi linaweza kuongeza nia yao ya kumnunua mshambuliaji wa Juventus, Vlahovic, ambaye ni sehemu ya mazungumzo magumu yanayojumuisha kuondoka kwa Romelu Lukaku.