Klabu ya Chelsea imeripotiwa kufanya fanya mazungumzo ya kutaka kumsajili Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana na klabu ya Ajax Amsterdam ya Uholanzi, Mohammed Kudus.
Klabu za Arsenal na Brighton pia zimeonesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, anayekadiriwa kuwa na thamani ya Pauni Milioni 40 baada ya kukataa ofa ya kuongeza mkataba mpya.
Kudus, ambaye almanusura ajiunge na Everton mwaka mmoja uliopita, alivutia kwenye Kombe la Dunia 2022 akiwa na Ghana.
Hili linakuja wakati kikosi hicho cha Mauricio Pochettino kikiwa kwenye mvutano na Brighton kuhusu kupatikana kwa nyota wa Pauni Milioni 100, Moises Caicedo, huku kocha Roberto De Zerbi akionesha wazi msimamo wake thabiti wa kutomruhusu raia huyo wa Ecuador kuondoka.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana alinyakuliwa na klabu hiyo ya Eredivisie mwaka 2020 kwa Pauni Milioni nane baada ya kuonesha kiwango kizuri katika klabu yake ya zamani ya FC Nordsjaelland.
Alianza maisha polepole pale Amsterdam, akijitahidi kusisitiza nafasi yake kwenye timu nyuma ya Anthony, ambaye aliondoka kwenda Manchester United mnamo mwaka 2022.
Kwa mujibu wa The Athletic, “The Blues’ wanakaribia kukubaliana na maslahi binafsi na mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ghana.
Kudus alikuwa wa pili kwa ubora katika msururu wa mabao, lakini baada ya Mbrazil huyo kuondoka, alifanikiwa katika klabu hiyo ya Uholanzi, akifunga mara 11 katika mechi 30 za ligi msimu uliopita.
Alikuwa muhimu kwa Ajax wakati wa mbio zao za Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka jana, akifunga katika mechi nne kati ya sita za mashindano hayo, haswa akifunga dhidi ya Liverpool kwenye Uwanja wa Anfield.
Uchezaji mzuri wa nyota huyo wa kutumainiwa umevutia hisia za klabu nyingi za Ligi Kuu England.
Erik ten Hag pia alikuwa anatazamia kutaka kumnunua kiungo wake huyo wa zamani, kabla ya United kumsajili Mason Mount.
Arsenal na Brighton ndizo klabu zilizopo kwenye foleni inayokua ya mahali ambapo mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ghana anahitajika.