Usajiliwa Kiungo Mshambuliaji kutoka DR Congo Chico Ushindi Wa Kubanza umempa jeuri Kocha Mkuu wa Young Africans Nasreddine Nabi, katika mbio za Ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu 2021/22.

Choco Ushindi alisajiliwa Young Africans wakati wa Dirisha Dogo mwezi Januari 2022, akitokea TP Mazembe ya nchini kwao DR Congo.

Kocha Nabi amesema kuwa licha ya kuwepo hatihati ya kumtumia Fei Toto aliye majeruhi kwa sasa, ana matumaini makubwa ya kumtumia Chico, kutokana na kuwa na sifa ya kucheza nafasi ya namba kumi.

Amesema anaamini uwezo mkubwa alionao Chico kutokana na kumfahamu baada ya kumfuatilia tangu akiwa klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.

Ameongeza kuwa Chico ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja namba 7, 10 na 11 hivyo uwepo wake katika timu, unampa nafasi kubwa ya kuwepo katika kikosi chake cha kwanza.

“Chico ana faida kubwa katika timu, hiyo ni kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi zaidi ya moja katika timu, hivyo ninaamini atatoa mchango mkubwa katika timu.

“Hivyo ushindani utaongezeka katika timu baada ya Chico kuja, hivi sasa kilichobakia kwake ni kuingia katika mfumo ambacho ni kitu kidogo, hilo ni jukumu langu ambalo nitalifanya,” amesema Nabi.

Tayari Choco ameshaitumikia Young Africans katika mchezo mmoja wa Ligi Kuu dhidi ya Polisi Tanzania, ulichezwa Jumapili (Januari 23) mjini Arusha, huku akitangulia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbuni FC.

Moallin akabidhiwa jumla Benchi la Ufundi Azam FC
Federico Chiesa ndio basi tena!