Rapa Chid Benz ambaye hivi karibuni ameonekana akiwa bega kwa bega na WCB huku akishikwa mkono na meneja wa Diamond, Babu Tale amesema kuwa yeye bado ni ‘La Familia’.

Chid amesema kuwa ingawa anafanya kazi kwa karibu na WCB, hajajiunga kwa namna yoyote na kundi hilo bali anafanya kazi tu na wasanii wake.

“No nimekwambia mimi ni La Familia na nafanya kazi na Lafamilia. Mimi ni Lafamilia lakini nimefanya kazi na wasanii wa WCB,” Chid Benz aliiambia East Africa TV. “Ni kama ambavyo ningeweza kufanya kazi na wasanii wa THT ina maana ungenambia kuwa mimi niko chini ya Boss wa THT?” Alihoji.

Chid ambaye hivi karibuni ameachia wimbo wake ‘Chuma’ akiwa na msanii wa WCB, Raymond amesema kuwa ataendelea kuwa ndani ya kundi lake la La Familia siku zote na kufanya kazi na wasanii walio chini ya lebel mbalimbali.

Katika hatua nyingine, Chid Benz amesisitiza kuwa yeye bado ndiye mfalme wa Hip Hop nchini na kwamba hata wasanii wenzake wanajua hilo.

JK: Haikuwa Rahisi kumshawishi Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM
Video: Cassim Mganga akitumbuiza katika Tamasha la ZIFF Zanzibar