Kiungo Mshambuliaji kutoka DR Congo Chico Ushindi Wakubanza, tangu ajiunge na timu hiyo amekuwa akikumbwa na majeraha ya mara kwa mara hali inayomfanya kushindwa kuonesha ubora ambao Wanayanga wana uhitaji.

Kiungo huyo aliyejiunga na Young Africans katika usajili wa dirisha dogo msimu huu akitokea TP Mazembe, majeraha makubwa yanayomsumbua ni kupata maumivu ya nyama za paja.

Hivi karibuni, nyota huyo, aliukosa mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Tanzania Bara ‘ASFC dhidi ya Geita Gold baada ya kupata majeraha hayo.

“Chico alipata majeraha ya nyama za paja akiwa mazoezini wakati kikosi kikijiandaa na mchezo wa michuano ya Shirikisho dhidi ya Geita Gold.”

“Unajua hayo majeraha yanaweza kukupata wakati wowote, lakini kwa sasa yupo fiti na ataanza mazoezi na timu, huenda akacheza mechi inayofuata dhidi ya Simba.” Imeeleza taarifa kutoka Young Africans

Dokta wa Yanga, Sheik Mngazija amesema: “Kuhusu suala la majeraha ya Ushindi (Chico) kwa sasa amepona na ataanza mazoezi na timu tutakapoanza maandalizi ya mchezo ujao.”

Katika michezo ya kimashindano aliyocheza, Chico Ushindi bado hajafunga bao.

Mashabiki Simba SC wamtisha Gabadinho
Kapombe: Tutapambana hadi mwisho