Timu ya taifa ya Chile, ipo kwenye hatari ya kuwakabili mabingwa wa kihistoaria wa dunia, timu ya taifa ya Brazil, bila ya kuwa na mshambuliaji wao Alexis Sanchez pamoja na kiungo Arturo Vidal.

Wawili hao, wana matarajio hafifu ya kucheza mchezo huo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, utakaochezwa hii leo, kufuatia kujitonesha majeraha walipokua kwenye mazoezi ya mwisho.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Chile, Jorge Sampaoli amesema kucheza ama kutokucheza kwa wachezaji hao muhimu katika kikosi chake, kunategemea na hali zao zitakavyoendelea hii leo kabla ya kipyenga hakijapulizwa.

Sanchez pamoja Vidal, wamekua na msaada mkubwa sana kwenye timu ya taifa ya Chile, kutokana na umahiri wao wa kucheza kwa kujituma wakati wote, na inaaminika kama wataukosa mchezo wa hii leo dhidi ya Brazil, huenda mambo yakabadilika na morari ikashuka kwenye kikosi cha Chile.

Hata hivyo kocha Sampaoli, amesema jambo hilo halimpi shida, kutokana na kuamini ana wachezaji wengi wenye uwezo wa kupambana na kikosi chochote duniani, hivyo taarifa yoyote atakayoipokea kutoka kwa daktari wa timu, atalipokea kwa mikono miwili.

Sanchez, alilazimika kutolewa uwanjani mwishoni mwa juma lililopita wakati wa mchezo wa ligi ya nchini England dhidi ya Man Utd katika kipindi cha pili, kufuatia maumivu wa nyonya yanayomsumbua.

Vidal, naye alikosa mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita katika ligi ya nchini Ujerumani kufuatia maumivu wa goti, ambapo FC Bayern Munich walipambana na Borussia Dortmund.

Gus Poyet Domínguez Ampigia Pande Sam Allardyce
Magufuli Amvaa Mbowe, Amuita Mzururaji